Siku ya Mbingu kujawa na sifa,
(One day when Heaven was filled with His praises)
Siku ya Mbingu kujawa na sifa,
Dhambi zilizidi duniani;
Yesu akaja azaliwe mtu,
Awe na watu ulimwenguni.
Alinipenda, alinifia,
Ameondoa na dhambi zangu;
Alifufuka nipewe haki,
Yuaja tena Mwokozi wangu.
Na siku moja walikwenda naye,
Wakamkaza Msalabani;
Aliumia, aliaibishwa
Siku hiyo wakamlaza chini
Kaburini alipumzika;
Matumaini yetu wenye dhambi,
Ni Mwokozi, kwake twaokoka.
Kaburi likashindwa kumshika;
Jiwe likatoka mlangoni,
Alifufuka kwa kushinda kwake,
Naye yuko mileie Mbinguni.
Siku moja atatujia tena;
Utukufu wake tutaona;
Atawaleta na wapenzi wetu;
Mwokozi wangu tutaonana.
No comments:
Post a Comment